Umri wa miaka 6-8
Umri wa miaka 9-12
Umri wa miaka 13-17

Ungependa kujua kuhusu faragha yako kwenye Google?

Umekuja mahali panapostahili! Soma maswali yanayoulizwa sana na watoto, kama vile jinsi mzazi wako anavyoweza kukusaidia kuhusiana na vitu vyako kwenye Google, maelezo ambayo Google hutumia na mengine mengi.

Wazazi, maelezo haya yanatumika tu kwa Akaunti za Google zinazodhibitiwa kupitia Family Link, za watoto walio na umri wa chini ya miaka 13 (au umri unaoruhusiwa katika nchi yako). Kwa maelezo zaidi, angalia Ilani ya Faragha na Sera yetu ya Faragha.

Ni nani anayedhibiti akaunti yangu?

Mzazi wako ndiye anayedhibiti Akaunti yako ya Google. Anaweza kutumia programu iitwayo Family Link kumsaidia kuidhibiti. Unaweza kudhibiti akaunti yako mwenyewe ukitimiza umri unaoruhusiwa.

Mzazi wako anaweza kufanya mambo kama vile:

 • Kuingia katika akaunti yako, kubadilisha nenosiri la akaunti yako au kufuta akaunti yako.
 • Kufunga simu au kompyuta kibao yako.
 • Kuona mahali simu au kompyuta kibao yako ilipo.
 • Kuchagua programu unazoweza kutumia.
 • Kuona muda unaotumia kwenye programu zako.
 • Kubadilisha vitu unavyoviona katika baadhi ya programu za Google, kama vile huduma ya Tafuta na Google, YouTube au Google Play.
 • Kuchagua Vidhibiti vya Shughuli zako. (Hii ni mipangilio inayohifadhi maelezo kuhusu mambo unayoyafanya kwenye Google.)
 • Kuchagua mipangilio na ruhusa za programu zako.
 • Kuchagua jina, siku ya kuzaliwa na maelezo mengine ya akaunti yako.
 • Kuchagua unachoweza kupakua au kununua katika baadhi ya bidhaa za Google, kama vile Google Play.

Google hutumia maelezo yangu vipi na kwa sababu gani?

Huenda tukahifadhi maelezo ambayo wewe au mzazi wako mnatupatia, kama vile jina lako na tarehe yako ya kuzaliwa. Pia tunahifadhi maelezo unapotumia programu na tovuti zetu. Tunajitahidi kuweka maelezo haya kwa usalama na tunayatumia kwa sababu tofauti — kama vile kufanya programu na tovuti za Google zikufae zaidi.

Ukisaidiwa na mzazi wako, pata maelezo zaidi kuhusu baadhi ya njia ambazo tunaweza kutumia maelezo yako:

 • Kuwezesha programu na tovuti zetu zifanye kazi: Kwa mfano, ukitafuta "paka wachanga" kwenye huduma ya Tafuta na Google, tunatumia maelezo yako kukuonyesha mambo yanayohusu paka wachanga.
 • Kuboresha programu na tovuti zetu: Kwa mfano, ikiwa kuna hitilafu, tunaweza kutumia maelezo kuirekebisha.
 • Kulinda Google, watumiaji wetu na umma: Tunatumia maelezo kuimarisha usalama wa watu mtandaoni.
 • Kuunda programu na tovuti mpya: Huwa tunajifunza jinsi watu wanavyotumia programu na tovuti zetu zilizopo ili tupate vidokezo kuhusu vitu vipya vya Google tunavyoweza kutengeneza.
 • Kukuonyesha vitu ambavyo huenda ukavipenda: Kwa mfano, ikiwa unapenda kutazama video za wanyama kwenye YouTube Kids, tunaweza kukuonyesha zingine kama hizo.
 • Kukuonyesha matangazo kulingana na vitu kama vile tovuti unayotumia.
 • Kuwasiliana nawe: Kwa mfano, huenda tukatumia anwani yako ya barua pepe kukutumia ujumbe. Muulize mzazi kila wakati kabla ya kufungua ujumbe kutoka kwa mtu usiyemjua.

Je, ninaweza kuiambia Google data itakayoihifadhi?

Ndiyo, unaweza kubadilisha baadhi ya mambo tunayohifadhi kukuhusu. Ukifanya mabadiliko kwenye baadhi ya mipangilio yako ya faragha, kama vile Vidhibiti vya Shughuli, tutamjulisha mzazi wako. Anaweza pia kukusaidia kubadilisha mipangilio yako.

Wewe na mzazi wako mnaweza kuona na kudhibiti baadhi ya maelezo kukuhusu na kuhusu Akaunti yako ya Google wakati wowote.

Je, Google hushiriki taarifa zangu binafsi na wengine?

Kuna sababu kadhaa zinazoweza kutufanya tushiriki taarifa zako binafsi, kama vile jina lako, nje ya Google. Tukishiriki taarifa hizi, huwa tunachukua hatua za kuhakikisha kwamba zimelindwa.

Huenda tukashiriki taarifa fulani binafsi:

 • Na mzazi na kikundi cha familia yako kwenye Google
 • Na kampuni tunazofanya kazi nazo
 • Mzazi wako anapotupatia idhini ya kuzishiriki
 • Tunapohitaji kuzishiriki kwa sababu za kisheria

Ni nani mwingine anayeweza kuona vitu ninavyoshiriki mtandaoni?

Chochote unachoshiriki mtandaoni, kama vile barua pepe au picha, kinaweza kuonekana na watu wengi. Shiriki tu na watu unaowaamini. Iwapo huna uhakika, mwulize mzazi au mwanafamilia.

Je, ungependa kupata maelezo zaidi? Mwombe mzazi akusaidie kusoma Sera yetu ya Faragha.

Ungependa kujua kuhusu faragha yako kwenye Google?

Umekuja mahali panapostahili! Hapa ndipo unaweza kupata maelezo ya jinsi Google inavyokusanya na kutumia maelezo unapotumia programu na tovuti zetu. Unaweza pia kupata maelezo kuhusu jinsi mzazi wako anavyoweza kukusaidia kudhibiti Akaunti ya Google na vifaa vyako.

Wazazi, maelezo haya yanatumika tu kwa Akaunti za Google zinazodhibitiwa kupitia Family Link, za watoto walio na umri wa chini ya miaka 13 (au umri unaoruhusiwa katika nchi yako). Kwa maelezo zaidi, angalia Ilani ya Faragha na Sera yetu ya Faragha.

Ni nani anayedhibiti akaunti yangu?

Kwa sasa, mzazi wako ndiye anayedhibiti Akaunti yako ya Google. Anaweza kutumia programu iitwayo Family Link kumsaidia kudhibiti akaunti yako hadi utakapotimiza umri unaoruhusiwa wa kudhibiti akaunti yako mwenyewe.

Mzazi wako anaweza kufanya mambo kama vile:

 • Kuingia katika akaunti yako, kubadilisha nenosiri la akaunti yako au kufuta akaunti yako.
 • Kuweka vikomo vya muda na wakati unaoweza kutumia vifaa vyako kama vile simu na kompyuta kibao.
 • Kuona mahali simu au kompyuta kibao yako ilipo.
 • Kuchagua programu unazoweza kutumia.
 • Kuona muda unaotumia kwenye programu zako.
 • Kudhibiti mipangilio ya maudhui ya baadhi ya programu na tovuti za Google, kama vile huduma ya Tafuta na Google, YouTube au Google Play. Mipangilio hii inaweza kubadilisha maudhui unayoweza kuyaona.
 • Kusimamia Vidhibiti vya Shughuli kwenye akaunti yako, kama vile Historia ya YouTube, ikiwa ni pamoja na kukuzuia usisimamie vidhibiti hivi wewe mwenyewe.
 • Kukagua ruhusa za programu kwenye simu au kompyuta kibao yako, kama vile kubaini iwapo programu zinaweza kutumia maikrofoni, kamera au anwani zako.
 • Kuangalia, kubadilisha au kufuta maelezo kuhusu akaunti yako, kama vile jina lako, jinsia au tarehe yako ya kuzaliwa.
 • Kuidhinisha upakuaji na ununuzi wako katika baadhi ya programu na tovuti za Google, kama vile Google Play.

Google hutumia maelezo yangu vipi na kwa sababu gani?

Kama ilivyo katika tovuti na programu nyingi, tunakusanya maelezo ambayo wewe au mzazi anatupatia, kama vile jina lako na tarehe ya kuzaliwa, na tunakusanya maelezo unapotumia programu na tovuti zetu. Tunajitahidi kuweka maelezo haya kwa usalama na tunayatumia kwa mambo kama vile kufanya bidhaa zetu zikufae zaidi. Kwa mfano, huwa tunakusanya data kwa ajili ya:

 • Kuwezesha programu na tovuti zetu zifanye kazi: Kwa mfano, ukitafuta "spoti" kwenye huduma ya Tafuta na Google, tunatumia maelezo yako kukuonyesha mambo yanayohusu spoti.
 • Kuboresha programu na tovuti zetu: Kwa mfano, ikiwa kuna hitilafu, tunaweza kutumia maelezo kuirekebisha.
 • Kulinda Google, watumiaji wetu na umma: Tunatumia maelezo kuimarisha usalama wa watu mtandaoni, kama vile kutambua na kuzuia ulaghai.
 • Kuunda programu na tovuti mpya: Huwa tunajifunza jinsi watu wanavyotumia programu na tovuti zetu zilizopo ili tupate vidokezo kuhusu bidhaa mpya za Google tunazoweza kutengeneza.
 • Kuweka mapendeleo ya maelezo kwa ajili yako, yaani kukuonyesha vitu ambavyo tunafikiri kwamba huenda ukavipenda. Kwa mfano, ikiwa unapenda kutazama video za wanyama kwenye YouTube Kids, tunaweza kukupendekezea video zingine kama hizo.
 • Kukuonyesha matangazo kulingana na vitu kama vile tovuti unayotumia.
 • Kuwasiliana nawe: Kwa mfano, huenda tukatumia anwani yako ya barua pepe kukutumia ujumbe, kama vile kunapotokea tatizo la usalama. Muulize mzazi kila wakati kabla ya kufungua ujumbe kutoka kwa mtu usiyemjua.

Je, ninaweza kuiambia Google data itakayoihifadhi?

Ndiyo, unaweza kubadilisha baadhi ya mambo tunayohifadhi kukuhusu. Kwa mfano, iwapo hutaki tuhifadhi Historia yako ya YouTube kwenye Akaunti yako ya Google, unaweza kuzima kipengele cha Historia ya YouTube. Ukibadilisha baadhi ya mipangilio yako ya faragha, kama vile Vidhibiti vya Shughuli, tutamjulisha mzazi wako. Anaweza pia kukusaidia kubadilisha mipangilio yako.

Wewe na mzazi wako mnaweza kuona na kudhibiti baadhi ya maelezo kukuhusu na kuhusu Akaunti yako ya Google wakati wowote.

Je, Google hushiriki taarifa zangu binafsi na wengine?

Kuna sababu kadhaa zinazoweza kutufanya tushiriki taarifa zako binafsi, kama vile jina lako na anwani yako ya barua pepe, nje ya Google. Tukishiriki taarifa hizi, huwa tunachukua hatua za kuhakikisha kwamba zimelindwa.

Huenda tukashiriki taarifa fulani binafsi:

 • Na mzazi na kikundi cha familia yako kwenye Google
 • Na kampuni tunazofanya kazi nazo
 • Mzazi wako anapotupa idhini ya kuzishiriki
 • Tunapohitaji kuzishiriki kwa sababu za kisheria

Ni nani mwingine anayeweza kuona vitu ninavyoshiriki mtandaoni?

Chochote unachoshiriki mtandaoni, kama vile barua pepe au picha, kinaweza kuonekana na watu wengi. Ukishiriki kitu mtandaoni, inaweza kuwa vigumu kukiondoa. Shiriki tu na watu unaowaamini. Iwapo huna uhakika, mwulize mzazi au mwanafamilia.

Je, ungependa kupata maelezo zaidi? Mwombe mzazi akusaidie kusoma Sera yetu ya Faragha.

Ungependa kujua kuhusu faragha yako kwenye Google?

Hapa ndipo unaweza kupata maelezo ya jinsi Google inavyokusanya na kutumia maelezo unapotumia programu na tovuti zetu. Unaweza pia kupata maelezo kuhusu jinsi mzazi wako anavyoweza kukusaidia kudhibiti Akaunti ya Google na vifaa vyako.

Maelezo haya yanatumika tu kwa Akaunti za Google zinazodhibitiwa kupitia Family Link, za watoto na vijana ambao hawajatimiza masharti ya umri wa chini unaohitajika kudhibiti akaunti zao wenyewe. Kwa maelezo zaidi, angalia Ilani ya Faragha na Sera yetu ya Faragha.

Je, mzazi wangu anaweza kusaidia kudhibiti akaunti yangu?

Mzazi wako anaweza kutumia programu inayoitwa Family Link kumsaidia kudhibiti vipengee fulani vya Akaunti yako ya Google. Kwa kutegemea kifaa chako, anaweza kufanya mambo kama vile:

 • Kuingia katika akaunti yako, kubadilisha nenosiri la akaunti yako au kufuta akaunti yako.
 • Kuweka vikomo vya muda na wakati unaoweza kutumia vifaa vyako.
 • Kuona mahali vifaa ambavyo umevitumia kuingia katika akaunti vilipo.
 • Kudhibiti programu zako na kuona muda unaozitumia.
 • Kudhibiti mipangilio ya maudhui ya baadhi ya programu na tovuti za Google, kama vile huduma ya Tafuta na Google, YouTube au Google Play. Mipangilio hii inaweza kubadilisha maudhui unayoweza kuyaona.
 • Kusimamia Vidhibiti vya Shughuli kwenye akaunti yako, kama vile Historia ya YouTube, ikiwa ni pamoja na kukuzuia usisimamie vidhibiti hivi wewe mwenyewe.
 • Kukagua ruhusa za programu kwenye kifaa chako, kama vile kubaini iwapo programu zinaweza kutumia maikrofoni, kamera au anwani zako.
 • Kuangalia, kubadilisha au kufuta maelezo kuhusu akaunti yako, kama vile jina lako, jinsia au tarehe yako ya kuzaliwa.
 • Kuidhinisha upakuaji na ununuzi wako katika baadhi ya programu na tovuti za Google, kama vile Google Play.

Google hukusanya na kutumia maelezo yangu vipi na kwa sababu gani?

Kama ilivyo katika tovuti na programu nyingi, tunakusanya maelezo ambayo wewe au mzazi anatupatia, kama vile jina lako na tarehe ya kuzaliwa, na tunakusanya maelezo unapotumia programu na tovuti zetu. Tunajitahidi kuweka maelezo haya kwa usalama na tunayatumia kwa mambo kama vile kufanya bidhaa zetu zikufae zaidi. Kwa mfano, huwa tunakusanya data kwa ajili ya:

 • Kulinda Google, watumiaji wetu na umma: Tunatumia data kuimarisha usalama wa watu mtandaoni, kama vile kutambua na kuzuia ulaghai.
 • Kutoa huduma zetu: Tunatumia data kutoa huduma zetu, kama vile kuchakata hoja unazotafuta ili kukupa matokeo.
 • Kudumisha na kuboresha huduma zetu: Kwa mfano, tunaweza kufuatilia bidhaa zetu zinapoacha kufanya kazi inavyopaswa. Kutambua hoja za utafutaji ambazo huendelezwa visivyo mara kwa mara hutusaidia kuboresha vipengele vya kikagua tahajia vinavyotumika katika huduma zetu mbalimbali.
 • Kubuni huduma mpya: Data hutusaidia kubuni huduma mpya. Kwa mfano, baada ya kuelewa jinsi watu walivyopanga picha zao katika programu ya Picasa, ambayo ilikuwa programu ya kwanza ya picha ya Google, tuliweza kubuni na kuzindua huduma ya Picha kwenye Google.
 • Kuweka mapendeleo ya maudhui, yaani kukuonyesha vitu ambavyo tunafikiri kwamba huenda ukavipenda. Kwa mfano, ikiwa unapenda kutazama video za spoti kwenye YouTube, tunaweza kukupendekezea video zingine kama hizo.
 • Kukuonyesha matangazo kulingana na maelezo kama vile tovuti unayotumia, hoja za utafutaji ulizoandika au jiji na jimbo lako.
 • Kupima utendaji: Tunatumia data kupima utendaji na kuelewa jinsi huduma zetu zinavyotumiwa.
 • Kuwasiliana nawe: Kwa mfano, huenda tukatumia anwani yako ya barua pepe kukutumia arifa tukitambua shughuli ya kutiliwa shaka.

Ninawezaje kuamua data inayohifadhiwa na Google?

Kwenye mipangilio yako, unaweza kudhibiti data tunayokusanya na jinsi data hiyo inavyotumiwa. Kwa mfano, iwapo hutaki tuhifadhi Historia yako ya YouTube kwenye Akaunti yako ya Google, unaweza kuzima kipengele cha Historia ya YouTube. Mzazi wako ataarifiwa ukibadilisha Vidhibiti vya Shughuli zako. Pata maelezo zaidi kuhusu mipangilio yako ya faragha

Unaweza kuona na kudhibiti baadhi ya maelezo kukuhusu na kuhusu Akaunti yako ya Google wakati wowote.

Je, Google hushiriki taarifa zangu binafsi na wengine?

Hatushiriki taarifa zako binafsi na kampuni, mashirika au watu binafsi nje ya Google isipokuwa katika hali chache kama vile tunapohitajika kisheria kufanya hivyo. Tukishiriki taarifa hizi, huwa tunachukua hatua za kuhakikisha kwamba zimelindwa.

Huenda tukashiriki taarifa fulani binafsi:

 • Na mzazi wako na kikundi cha familia yako kwenye Google.
 • ​​Wewe na mzazi wako mnapotupatia ruhusa au kwa sababu za kisheria. Tutashiriki taarifa binafsi nje ya Google ikiwa tunaamini kuwa kufanya hivyo ni muhimu kwa:
 • Kutimiza sheria yoyote husika, kanuni, mchakato wa kisheria au ombi la kiserikali linaloweza kutekelezwa.
 • Kutekeleza Sheria na Masharti yanayotumika, ikiwemo uchunguzi wa ukiukaji unaoweza kutokea.
 • Kugundua, kuzuia au kushughulikia ulaghai, usalama au masuala ya kiufundi.
 • Kulinda dhidi ya ukiukaji wa haki, madhara kwa mali au usalama wa Google, watumiaji wetu au umma kama inavyohitajika au kuruhusiwa na sheria.
 • Kwa uchakataji wa nje. Tunatoa taarifa binafsi kwa kampuni tunazofanya kazi nazo ili ziweze kuchakata data kulingana na maagizo tunayozipatia. Kwa mfano, tunatumia kampuni za nje ili zitusaidie kutoa usaidizi kwa wateja na tunalazimika kushiriki taarifa binafsi na kampuni hizo ili ziweze kujibu maswali ya watumiaji.

Ni nani mwingine anayeweza kuona vitu ninavyoshiriki, kama vile picha, barua pepe na hati?

Unaweza kuchagua kushiriki maudhui mahususi na watu wengine katika programu na tovuti za Google unazotumia.

Usisahau kwamba ukishiriki, watu wengine wanaweza kushiriki tena, hata katika programu na tovuti zilizo nje ya Google.

Unaweza kufuta maudhui yako mwenyewe kwenye akaunti yako wakati wowote, lakini hatua hii haifuti nakala ambazo umezishiriki tayari.

Kuwa makini kuhusu maudhui unayoyashiriki na ushiriki tu na watu unaowaamini.

Ili upate maelezo zaidi kuhusu mada hizi, unaweza kuangalia Sera yetu ya Faragha wakati wowote.