Usimamizi wa akaunti za watoto na vijana

Wazazi wanaweza kuwasaidia vijana wao kufanya maamuzi bora mtandaoni kwa kusimamia vifaa na Akaunti zao za Google. Kwa kutumia programu ya Family Link, wazazi wataweza kufanya mambo kwenye vifaa vya mtoto wao vinavyooana kama vile:

  • Kuzuia au kuruhusu programu au tovuti fulani
  • Kuangalia programu anazotumia mtoto wao na muda anaozitumia
  • Kufunga vifaa wakati wa kupumzika, kusoma au kulala

Kabla hujaanza

  • Kuweka mipangilio ya usimamizi huenda kukachukua takriban dakika 10
  • Mzazi na kijana lazima wawe na Akaunti ya Google kila mmoja
Programu za Google
Menyu kuu